Maelekezo ya Usajili kwenye mfumo wa ACMS

Announced by Tarime Sda on 20 Dec 2017

Washiriki wote ambao wameshabatizwa na hawajajaza fomu ya ACMS mnaombwa kuchukua fomu hizo katika ofisi ya katibu wa Kanisa na kuanza kujaza hizo fomu na kuzirudisha ofisini kwa ajili ya kuingizwa mtandaoni. 

  Tafadhali zingatia yafuatayo-:

1. Kama ulishawahi kujaza fomu hiyo usirudie tena kuijaza labda tu kama hukuingizwa kwenye mfumo huo kwa sababu maalumu.
2. Uwe mshiriki wa Kanisa La Tarime Central
3 Uwe umeshabatizwa
4. Uhakikishe kwamba umeshaleta ushirika wako katika Kanisa hilo.
5. Jaza taarifa zako zilizo sahihi ikiwemo jina ulilotumia wakati wa kubatizwa.
6. Jaza taarifa kulingana na jina lililopokelewa katika Kanisa la Tarime Central wakati wa uhamisho wa ushirika wako.